Trump aagiza kusitishwa kwa usambazaji wa Dawa za UKIMWI kwa nchi maskini

0
Trump aagiza kusitishwa kwa usambazaji wa Dawa za UKIMWI kwa nchi maskini

RAIS wa Marekani, Donald Trump ameagiza kusitishwa usambazaji wa dawa za Ukimwi, malaria na kifua kikuu kwa nchi zinazopewa misaada na Shirika la Maendeleo la Marekani (USAID).

Agizo hilo limetolewa leo Januari 28, 2025 huku hatua hiyo ikilenga kupitia upya miradi mbalimbali ya misaada lakini imeibua wasiwasi mkubwa miongoni mwa wataalamu wa afya na mashirika ya kibinadamu. Kwa mujibu wa duru za kimataifa, agizo hilo linatarajiwa kuathiri mamilioni ya watu wanaotegemea huduma za matibabu kupitia programu kama Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na Ukimwi (PEPFAR).

Mpango huo, ulioanzishwa mwaka 2003, umeokoa zaidi ya maisha ya watu milioni 25 barani Afrika huku mashirika yanayotoa msaada, likiwamo la Chemonics, yakidai hatua hiyo itavuruga upatikanaji wa dawa na huduma kwa watu walioko hatarini zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *