Mbunge wa viti maalumu Halima Idd amefariki dunia akipatiwa matibabu

Mbunge wa viti maalumu Halima Idd amefariki dunia akipatiwa matibabu
Image with Link Description of Image

Mbunge wa viti maalumu aliyekuwa akiwakilisha kundi la Wafanyakazi wa Sekta binafsi na Umma, Halima Idd amefariki dunia leo  Jumapili, Januari 18, 2026 akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, jijini Dar es Salaam.

Taarifa za kifo hicho zimetolewa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Zungu. Taarifa hiyo imeeleza kuwa mazishi ya mbunge huyo yatafanyika leo kwenye makaburi ya  Kibada kwa Dole, Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Image with Link Description of Image
Image with Link Description of Image