Msimamo Kundi la Simba Kombe la Shirikisho CAF 2024/2025
Ushindi wa mabao 2-0 waliopata Simba dhidi ya CS Constantine katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika umeifanya simba kumaliza vinara wa kundi A.
Mchezo ulianza kwa kasi kwa Simba kuliandama lango la Constantine huku wakitengeneza nafasi kadhaa ambazo hata hivyo hawakuzitumia.
Katika dakika zote 45 za kipindi cha kwanza wageni Constantine walizitumia kujilinda huku wakifika mara mbili langoni wa Simba huku simba ikimiliki sehemu kubwa ya mchezo.
Kibu Denis aliipatia Simba bao la kwanza dakika ya 60 kwa shuti kali nje ya 18 baada ya kumalizia pasi ya kisigino iliyopigwa na Elie Mpanzu.
Leonel Ateba aliipatia Simba bao la pili dakika ya 80 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na mlinzi wa kulia Shomari Kapombe.
Ushindi huu umeifanya Simba kufikisha alama 13 ikiwa kileleni mwa msimamo baada ya kucheza mechi sita
X1: Camara, Kapombe, Zimbwe Jr (Nouma 84′) Che Malone, Hamza, Kagoma (Mzamiru 89′), Kibu, Ngoma (Fernandez 84′), Ateba (Balua 89′), Ahoua (Chasambi 84′), Mpanzu
Walioonyeshwa kadi: Kibu 8′ Kagoma 85′
X1: Zakaria, Laid, Benchaira, Baouche, Benchaa (Temine 66′), Dib (Tehar 66′), Meddahi, Merbah, Abraham.(Belhocini 45′), Rebiai, Boudrama
Walioonyeshwa kadi: Baouche 10′ Merbah 34′ Rebiai 61′
Msimamo Kundi la Simba Kombe la Shirikisho CAF 2024/2025
Nafasi | Klabu | ||||||||
1 | Simba | 6 | 4 | 1 | 1 | 8 | 4 | 4 | 13 |
2 | CS Constantine | 6 | 4 | 0 | 2 | 12 | 6 | 6 | 12 |
3 | Bravos do Maquis | 6 | 2 | 1 | 3 | 7 | 14 | -7 | 7 |
4 | CS Sfaxien | 6 | 1 | 0 | 5 | 7 | 10 | -3 | 3 |