Habari kuu za Dunia leo (VIDEO)
Karibu kwenye Mkusanyiko wa habari kuku za dunia leo, Habari na matukio mbali mbali yaliyojiri kutoka kona mbali mbali duniani
UKRAINE: Ukraine yatazamiwa kupokea dola milioni 225 zaidi za msaada wa kijeshi kutoka Marekani huku nchi nyingine wanachama wa Jumuiya ya kujihami ya NATO wakiahidi kuipa Ukraine msaada zaidi
Katika siku ya mwisho ya mkutano wa kilele wa nchi wanachama wa Jumuiya ya kujihami ya NATO mjini Washington hapo jana Alhamis, Rais wa Marekani alitangaza kitita hicho cha fedha kwa ajili ya msaada wa kijeshi kwa Ukraine na pia alisisitiza azma ya nchi yake ya kuendelea kuiunga mkono Ukraine katika juhudi zake za kujilinda na uvamizi wa Urusi.
ISRAEL: Maafisa katika eneo linalodhitiwa na Hamas wamesema takriban miili 60 imepatikana kwenye vifusi katika viunga vya mji wa Gaza. Hii baada ya jeshi la Israel kutangaza kusitisha operesheni yake katika eneo hilo.
Hii baada ya jeshi la Israel kutangaza kusitisha operesheni yake katika eneo hilo. Huku haya yakijiri rais wa Marekani Joe Biden amesema mazungumzo juu ya mpango unaowezekana wa kusitisha mapigano “yanapiga hatua.”
MAREKANI: Rais Joe Biden amesisitiza siku ya Alhamisi kuwa atawania muhula mwingine wa urais na kumshinda Donald Trump huku makosa kadhaa ya aibu kwenye mkutano wa kilele wa NATO yakitia mashaka mapya juu ya uwezo wake wa kuongoza
Mkusanyiko wahabari zote kamili Tazama Video hapa chini