Japan yaipa Tanzania msaada wa Tsh Bilioni 8.9 kwa ajili ya mradi wa ukarabati wa Bandari ya Kigoma

0
Japan yaipa Tanzania msaada wa Tsh Bilioni 8.9 kwa ajili ya mradi wa ukarabati wa Bandari ya Kigoma

Japan yaipa Tanzania msaada wa Tsh Bilioni 8.9 kwa ajili ya mradi wa ukarabati wa Bandari ya Kigoma

Tanzania imepokea msaada wa nyongeza wa Yen za Japan milioni 548 sawa na shilingi bilioni 8.9 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa ukarabati wa Bandari ya Kigoma baada ya marekebisho ya mikataba miwili ya msaada kati ya Tanzania, Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) na Ubalozi wa Japan.

Mikataba ya marekebisho ya msaada imesainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, Balozi wa Japan nchini Tanzania, Yasushi Misawa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan Tanzania, Bw. Hitoshi Ara, kwa niaba ya Japan.

Akizungumza baada ya kusainiwa kwa marekebisho ya mikataba hiyo, Dkt. Mwamba alisema kuwa, awali Serikali ya Japan kupitia mikataba iliyosainiwa Februari 4, 2022 ilitoa msaada wa Yen za Japan bilioni 2.73 sawa na shilingi bilioni 44.42 kwa ajili ya ukarabati wa Bandari hiyo.

“Jumla ya msaada uliotolewa na Serikali ya Japan unakuwa Yen za Japan bilioni 3.27 sawa na shilingi bilioni 53.35, ambapo fedha zilizoongezwa zinalenga kuziba pengo lililotokana na kuporomoka kwa thamani ya Yen za Japan na shilingi ya Tanzania ikilinganishwa na dola ya Marekani”, alieleza Dkt. Mwamba.

Alisema kuwa Mradi huo, utaboresha usalama na ufanisi wa shughuli za upakiaji wa abiria na upakuaji wa mizigo kwa kukarabati jengo la abiria la Bandari ya Kigoma na ujenzi wa ghala la kuhifadhia mizigo litakalo gharamiwa na Serikali ya Tanzania na kujenga barabara unganishi za kuingia na kutoka bandarini ambako kutachangia kuimarika kwa biashara na usafirishaji katika maeneo husika.

Vilevile Dkt. Mwamba alisema kuwa upatikanaji wa fedha hizo ni mwendelezo wa ufadhili kutoka Serikali ya Japan katika miradi ya maendeleo ambapo Tanzania inanufaika katika maeneo ya sekta za Kilimo, Maji, Afya, Nishati, Usafirishaji, uendelezaji wa miji, elimu na Usimamizi wa Fedha za Umma.

Aidha, Dkt. Mwamba ameihakikishia Serikali ya Japan utayari wa Tanzania chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuendelea kuimarisha ushirikiano kwa maendeleo ya wananchi wa pande zote na kwamba itachukua hatua zote muhimu kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kikamilifu ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Kwa upande wake Balozi wa Japan nchini Tanzania, Yasushi Misawa, alisema kuwa wametoa msaada wa fedha za mradi wa ukarabati wa Bandari ya Kigoma kwa kuwa utasaidia katika ukuaji wa uchumi na masuala ya kijamii.

Alisema kutokana na kushuka kwa kasi kwa viwango vya ubadilishaji wa fedha kwa miaka ya hivi karibuni na kupanda kwa gharama za bidhaa na mafuta kutokana na mgogoro wa Ukraine na Urusi, Serikali yake ilitambua kutakuwa na ukosefu wa fedha katika mipango iliyokuwa imewekwa awali ndio sababu ya kuongeza fedha za mradi huo.

Alisema kuwa Bandari hiyo ni kitovu cha usafirishaji katika nchi za Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Zambia ikichochewa na miundombinu ya barabara na reli.

Balozi Misawa, alisema nchi yake inashirikiana na nchi mbalimbali katika utekelezaji wa miradi ili kukuza Uchumi kupitia miundombinu madhubuti na kuongeza ushirikiano na anaamini kupitia marekebisho ya mikata hiyo, mradi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *