Meli mbili za mafuta za Urusi zimeharibika vibaya katika Bahari Nyeusi
Meli mbili za mafuta za Urusi zimeharibika vibaya katika Bahari Nyeusi, na kusababisha mafuta kumwagika, mamlaka nchini Urusi imesema.
Picha zilizotolewa na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Uchukuzi Kusini mwa Urusi zilionyesha moja ya meli ikiwa imeharibika kabisa, huku mafuta yakionekana majini.
Meli zote mbili zinaaminika kuanza kuyumba kabla ya kuzama baharini.
Mfanyakazi mmoja aliripotiwa kufa maji.
Tukio hilo lilitokea katika Mlango-Bahari wa Kerch, unaotenganisha Urusi na Crimea – rasi ya Ukraine iliyoshikiliwa kinyume cha sheria na Urusi tangu mwaka 2014.
Operesheni ya uokoaji iliyohusisha boti inayovuta nyingine, iliokoa wafanyakazi 13 kutoka kwa meli moja ya mafuta, kabla ya kusitishwa kuendesha shughuli zake kutokana na hali mbaya ya hewa.
Wafanyakazi 14 waliosalia ndani ya meli ya pili wanasemekana kuwa na “kila kitu muhimu kwa ajili ya kuokoa maisha yao tena kwa haraka”, lakini walionekana kusitisha safari yao kwanza hadi hali itakapoimarika.
Rais Vladimir Putin ameamuru jopo kazi kuundwa kushughulikia tukio hilo, linaloongozwa na Naibu Waziri Mkuu Vitaly Savelyev – na mamlaka inachunguza kilichotokea.
Uagizaji wa mafuta ya Urusi umewekewa vikwazo na washirika wa Ukraine tangu Kremlin ilipoamuru uvamizi wa Ukraine mnamo mwezi Februari 2022.