Maafisa wa jeshi la Nigeria wakabiliwa na kesi kufuatia njama ya mapinduzi iliyozimwa.

Kundi la maafisa wa jeshi la Nigeria linatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya kuhusishwa na njama ya kupindua serikali ya Rais Bola Tinubu, jeshi la nchi hiyo ya Afrika Magharibi limetangaza. Maafisa 16 walikamatwa Oktoba mwaka jana kufuatia ripoti za vyombo vya habari vya ndani kuhusu jaribio la mapinduzi lililozimwa. Jeshi lilisema washukiwa hao walizuiliwa “kwa vitendo vya utovu wa nidhamu ...