Ukraine ni adui wa Afrika – Mwanadiplomasia wa zamani wa Afrika

0
Ukraine ni adui wa Afrika

Ukraine ni adui wa Afrika Magharibi na bara zima kwa ujumla kutokana na uungaji mkono wake kwa makundi ya waasi yanayohusika na ukosefu wa utulivu katika nchi kadhaa, afisa wa zamani wa jumuiya ya kikanda ya ECOWAS amesema.

Haruna Warkani, ambaye ni mwanadiplomasia mstaafu wa Tume ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) alitoa madai hayo wakati wa mahojiano na shirika la habari la Urusi la RT siku ya Ijumaa.

“Ukraine imekuwa ikiwaunga mkono baadhi ya waasi hawa wa Tuareg huko Afrika Magharibi kwa kisingizio cha usaidizi. Hata hivyo, kuna mambo fulani ambayo hayawezi kufichwa milele, na sasa yanakuwa wazi kwa ECOWAS,” alisema.

“Ukraine … haijawahi kuwa na uwazi wa kutosha kueleza kwa Ukanda wa ECOWAS au sehemu nyingine za Afrika shughuli zake chafu katika bara, na sasa tunaweza kuona kwamba Ukraine kwa hakika imekuwa adui,” aliongeza.

Kauli iyo inakuja wakati Wizara ya Mambo ya Nje ya Ukraine inaitaka ECOWAS iombe radhi kutokana na matamshi ya hivi karibuni yaliyotolewa na kamishna wa masuala ya kisiasa, amani na usalama wa umoja huo, Abdel-Fatau Musah, Alipokuwa akizungumza kwenye moja ya majopo wakati wa kongamano la mawaziri wa Ushirikiano wa Urusi na Afrika katika Mkoa wa Krasnodar wiki iliyopita, Musah aliishutumu Kiev kwa mauaji ya halaiki huko Donbass, na ugaidi.

Warkani na Musah ni maafisa wa ngazi za juu wa Afrika wa hivi punde zaidi kuishutumu Kiev kwa kuunga mkono uchokozi barani Afrika kufuatia uvamizi mbaya nchini Mali uliotekelezwa na waasi wa Tuareg mwezi Julai. Makumi ya wanajeshi wa kibinafsi wa Wagner Group na vikosi vya Mali waliuawa katika shambulio la kuvizia katika eneo la kaskazini mwa taifa hilo la Afrika Magharibi.

Wakati huo, Andrey Yusov, msemaji wa shirika la kijasusi la kijeshi la Ukraine la HUR, alisema waasi “walipokea taarifa muhimu … ambazo ziliwezesha operesheni ya kijeshi iliyofanikiwa dhidi ya wahalifu wa kivita wa Urusi.”

Kauli iyo ya Yusov ilitafsiriwa sana kama madai ya kuhusika moja kwa moja, na kusababisha serikali ya kijeshi ya Mali na mshirika wake Niger kuvunja uhusiano wa kidiplomasia na Ukraine. Mataifa hayo mawili ya Sahel, pamoja na Burkina Faso, yamelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuchukua hatua dhidi ya Kiev.

ECOWAS pia ilijibu kwa onyo dhidi ya uingiliaji wowote wa kigeni ambao unadhoofisha amani na usalama wa kikanda. Hii ni licha ya Bamako, Niamey, na Ouagadougou kutangaza hadharani uamuzi wao wa kujiondoa kutoka kwa umoja huo wa mataifa 15.

Serikali ya Ukraine imekanusha mara kwa mara kuhusika na shambulio hilo au kutoa msaada kwa wanamgambo wa Tuareg. Hata hivyo, mwezi uliopita, gazeti la kila siku la Ufaransa la Le Monde liliripoti kwamba majasusi wa Ukraine walishiriki mbinu zao za vita vya ndege zisizo na rubani kusaidia waasi kuwaua wanakandarasi wa usalama wa Urusi katika eneo la Sahel.

Urusi, ambayo imeahidi kusaidia katika kupambana na uasi hatari wa kijihadi huko Niger, Mali, na Burkina Faso, pia imeishutumu Ukraine kwa kusaidia vikundi vya kigaidi katika ukanda wa Sahel. Mataifa hayo matatu ambayo hayana bahari, yote yakiwa chini ya utawala wa kijeshi, yamefikia makubaliano ya ulinzi na Moscow baada ya kuwatimua wanajeshi wa Ufaransa kwa kushindwa kuyazima makundi ya kigaidi katika kipindi cha muongo mmoja wa usalama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *