Usajili Yanga 2024: Yanga yanasa Saini ya kiungo Duke Abuya raia wa Kenya
MASHINE ya Kusaga na Kukoboa Duke Abuya raia wa Kenya ambaye ni kiungo aliyekuwa ndani ya Singida Black Stars atakuwa kwenye anga la kimataifa na uzi wa kijani na njano katika kikosi cha Miguel Gamondi Yanga.
Yanga chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi inafanya maboresho makubwa kuelekea msimu mpya ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kitaifa na kimataifa.
Duke Abuya anaingia kwenye orodha ya nyota watakaokuwa na kazi kupeperusha bendera ya Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ndani ya kikosi cha Yanga.
Yanga kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika wana kazi ya kusaka ushindi dhidi ya Vital’O ya Burundi kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali.
Baada ya droo kuchezwa nchini Misiri Julai 11 2024, Yanga itaanzia ugenini kusaka ushindi kwenye mchezo wa kimataifa.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kati ya Agosti 16-18 marudiano Bongo itakuwa kati ya Agosti 23-25.
Vijana hao wa mitaa ya Jangwani wataanzia ugenini kwenye mchezo ambao utachezwa kati ya Agosti 16-18, 2024 na kurudiana kati ya Agosti 23-25.
Klabu ya Yanga imesajili wachezaji kibao wenye majina mkubwa na uwezo uwanjani, kuna Clatous Chama, Prince Dube, Chadrack Boka, Aziz Andabwile, na sasa Duke Abuya.
Wachezaji wanaohusishwa zaidi kujiunga na Simba, ni Jean BALEKE aliyewahi kucheza Simba kwa msimu mmoja na nusu akifunga jumla ya mabao 16, kisha akatimkia kwenda klabu ya Al Ittihad ya Libya.