Urusi Kuliondoa Kundi la Taliban kwenye Orodha ya makundi ya Kigaidi

0
Urusi Kuliondoa Kundi la Taliban kwenye Orodha ya makundi ya Kigaidi

Moscow italiondoa kundi la Taliban kwenye orodha ya mashirika ya kigaidi, Zamir Kabulov, mjumbe wa rais wa Urusi nchini Afghanistan, aliwaambia waandishi wa habari siku ya Ijumaa. Mabadiliko hayo pia yalithibitishwa na Aleksandr Bortnikov, mkuu wa Huduma ya Usalama ya Shirikisho (FSB), ambayo ina jukumu la kupambana na vitisho vya ugaidi.

Urusi ilikuwa miongoni mwa mataifa ya kwanza kuanzisha mawasiliano na kundi la Taliban baada ya kunyakua mamlaka nchini Afghanistan mwaka wa 2021. Hata hivyo Urusi haijalitambua rasmi kundi hilo kama jeshi linaloongoza nchini humo.

Kundi hilo lilichukua madaraka huko Kabul wakati wa hatua ya mwisho ya kuondoka kwa wanajeshi wa Marekani, ambayo ilimaliza ukaliaji wa miaka 20 wa Nchi za Magharibi uko Afghanistan. Serikali ya Rais Ashraf Ghani iliyokuwa inayoungwa mkono na Washington iliikimbia nchi hiyo, pamoja na raia wengi waliowasaidia Wamarekani.

Mnamo Mei, Kabulov alielezea Taliban kama “hakika sio maadui wetu.” Akizungumza na waandishi wa habari siku ya Ijumaa, mwanadiplomasia huyo mkuu alisema kuwa Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi na FSB wanafanya kazi na mashirika mengine ya serikali kurasimisha kuondolewa kwa Taliban kwenye orodha ya kigaidi ya kitaifa.

Uamuzi wa kimsingi kuhusu suala hili tayari umeshatolewa na uongozi wa Urusi,” alisema Kabulo na kuongeza kuwa taratibu zote za kisheria zinapaswa kuruhusiwa. Itahitaji “kazi ya uadilifu ya wanasheria, bunge na mashirika mengine ya serikali,” Kabulov alisema. Alionyesha matumaini kwamba “uamuzi wa mwisho utatangazwa katika siku za usoni.”

Mkuu wa FSB alisema Ijumaa kwamba Moscow inakamilisha kuwaondoa Taliban kutoka kwenye orodha nyeusi. Kulingana na Bortnikov, hatua hiyo ingefungua njia kwa ajili ya “ushirikiano wa kivitendo” na kundi hilo, ikiwa ni pamoja na mapambano dhidi ya uhalifu uliopangwa na ISIS-K, ambalo ni kundi chipukizi la kikanda la Islamic State (IS, zamani ISIS).

Kundi la ISIS-K liimedai kuhusika na mashambulizi kadhaa nchini Urusi mwaka huu, ikiwa ni pamoja na kuvamia ukumbi wa muziki nje ya Moscow mwezi Machi na kusababisha vifo vya watu 145.

Urusi iliwaorodhesha kundi la Taliban mwaka wa 2003 kama kundi la kigaidi. Mamlaka ilisema wakati huo kwamba kundi hilo lilihusishwa na waasi wa Kiislamu katika eneo la kaskazini la Caucasus na lilihusika na utekaji nyara wa ndege ya raia wa Urusi mwaka 1995.

Mtazamo wa Moscow kuelekea kikundi hilo ulianza kubadilika baada ya waasi kushindwa kwa kiasi kikubwa nyumbani. Mabadiliko hayo yaliimarishwa zaidi na kuongezeka kwa harakati za kundi la IS katikati ya miaka ya 2010.

Rais Vladmir Putin alisema mwezi Julai kwamba kundi la Taliban lilikuwa linaidhibiti Afghanistan. “Kwa maana hii, Talib ni washirika wetu katika mapambano dhidi ya ugaidi,” Putin alisema, akiongeza kwamba Moscow ilipokea “ishara fulani” kwamba kundi hilo liko tayari kwa ushirikiano.

Waziri wa Mambo ya Nje Sergey Lavrov alisema mwezi Juni kwamba Urusi haitaitambua serikali ya Taliban hadi itimize masharti kadhaa, ikiwa ni pamoja na dhamira ya kupambana na biashara ya dawa za kulevya na ugaidi, na “kuheshimu haki za msingi za mataifa  yote ya Afghanistan.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *