Kroatia ambayo ni mwanachama wa NATO imekataa kupeleka wanajeshi Ukraine

Kroatia ambayo ni mwanachama wa NATO imekataa kupeleka wanajeshi Ukraine

Rais wa Kroatia Zoran Milanovic amekataa kuchangia wanajeshi kwa kamandi ya NATO kwa ajili ya kutoa msaada wa kijeshi kwa Kiev, akihoji kwamba hii itaivuta Zagreb – Krotia katika mzozo wa moja kwa moja na Moscow.

Jamhuri hiyo ya zamani ya Yugoslavia imekuwa mwanachama wa muungano wa NATO unaoongozwa na Marekani tangu mwaka 2009. Serikali yake ya mrengo wa kulia imetuma silaha na helikopta pekee nchini Ukraine, kutokana na pingamizi la rais huyo ambaye ni mwanachama wa social democtrats.

Image with Link Description of Image

“Wakati mimi ni rais na amiri jeshi mkuu, wanajeshi wa Kroatia, maafisa na NCO hawatashiriki katika shughuli ambazo zitaiingiza Kroatia katika vita,” Milanovic alisema Alhamisi.

Milanovic amekataa kuchangia mwanajeshi yeyote kwa kamandi ya Msaada wa Usalama na Mafunzo ya NATO kwa Ukraine (NSATU), ambayo kambi hiyo ilianzishwa kwa madhumuni ya kuratibu misaada ya kijeshi kwa Kiev. Kroatiia ilitakiwa kutuma maafisa wachache kuungana na wanajeshi 700 wa NSATU huko Wiesbaden, Ujerumani.

Waziri Mkuu wa Croatia Andrej Plenkovic amemshutumu rais huyo kwa “kuzidi kuitenga Croatia katika eneo la kimataifa na kuharibu uaminifu wake kama mwanachama wa NATO.”

Wakati huo huo, NATO imemkumbusha Milanovic kwamba amri hiyo ilikubaliwa katika mkutano wa kilele wa Julai mjini Washington na kwamba haitahusisha kutuma wanajeshi wowote nchini Ukraine. Jumui iyo ya NATO inayoongozwa na Marekani imesema kuwa kutumia mamia ya mabilioni ya dola kwa silaha, kutoa mafunzo na kusambaza juhudi za vita za Kiev haifanyi jumuiya iyo kuwa sehemu ya mzozo na Urusi.

“Iwe ni askari mmoja au mia, popote walipo, hii itakuwa amri ya moja kwa moja kwa upande unaopigana vita ambao si mwanachama wa NATO, na upande uo uko nje ya mipaka kwa maslahi ya kitaifa ya Kroatia,” Milanovic alijibu Alhamisi kwamba “Croatia ina wajibu wa kusaidia washirika na wanachama wa NATO, na tumekuwa tukifanya ivo.  Menggine ni kushiriki katika vita, ambayo sitaruhusu.” alisema rais huyo.

Rais uyo wa Kroation Alikumbusha kambi hiyo ya NATO kwamba Kroation imedhihirisha kujitolea kwake kwa karibu maradufu idadi ya wanajeshi wa Croatia katika kikosi cha mpaka cha NATO, kutoka 300 hadi 520.

Rais uyo akaongeza kuwa “Ninajibu kwa watu wa Croatia pekee, sio Washington na Brussels,”

Chini ya katiba ya Croatia, Milanovic ana haki ya kuzuia kupelekwa kwa wanajeshi nje ya nchi. Baraza la mawaziri linaweza kumpindua rais kwa kura ya thuluthi mbili katika bunge hilo, lakini muungano unaotawala unaungwa mkono na wabunge 78 pekee kati ya 151.

Milanovic kwa muda mrefu amekosoa sera ya NATO ya kuipa Ukraine silaha ili kupigana dhidi ya Urusi. Pia amekashifu jinsi Umoja wa Ulaya unavyoshughulikia nchi wanachama kama Poland na Hungary, na kuishutumu Brussels kwa kuichukulia Kroatia kama mtoto “mchanga”.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top