Korea kaskazini kupata tani 700000 za mchele kwa kupeleka silaha na wanajeshi Urusi
Gazeti la Korea Kusini la Korea Herald linaripoti, likimnukuu balozi wa zamani wa Korea Kusini nchini Urusi, kwamba badala ya usambazaji wa risasi na kutuma wanajeshi kushiriki katika vita vya Urusi na Ukraine, viongozi wa DPRK watapokea kutoka Moscow takribani tani 600-700 za mchele kwa mwaka na upatikanaji wa teknolojia ya anga.
Balozi wa zamani Wi Song-lak, ambaye alipokea taarifa kutoka kwa kamati ya kijasusi ya Korea Kusini, alisema kwamba siku za nyuma Moscow iliipatia Pyongyang tani 50,000 hadi 100,000 za mchele kwa mwaka, lakini sasa mahitaji yataongezeka hadi 600,000- tani 700,000.
Korea Kaskazini inasema inazalisha takribani tani milioni 4 za nafaka kila mwaka, lakini hiyo ni takribani tani milioni 1 pungufu ya kile inachohitaji, Wi Song-lak alisema.
Kwa hivyo vifaa kutoka Urusi vinaweza kusaidia Pyongyang kujaza upungufu wake wa nafaka kwa zaidi ya nusu. Urusi pia inaisaidia Pyongyang, ambayo inajiandaa kurusha satelaiti mpya ya kijasusi, yenye teknolojia ya hali ya juu ya anga, kulingana na maafisa wa Korea Kaskazini.
Lakini sehemu muhimu zaidi ya makubaliano na Moscow, kulingana na balozi wa zamani, ni ukweli kwamba Pyongyang ilipata msaada wa kijeshi wa Urusi katika tukio la vita kwenye Peninsula ya Korea.
“Korea Kaskazini, ilipigana upande wa Urusi. Ikiwa vita vitatokea kwenye Rasi ya Korea, Korea Kaskazini inaweza kutegemea Urusi kuja kusaidia,” Wie alisema.
Kulingana na mamlaka ya Ukraine na Magharibi, DPRK imetuma takribani wanajeshi 10,000 nchini Urusi, ambao hivi karibuni wanaweza kutumwa kwenye vita vya Urusi na Ukraine.
Miji mikuu ya Kyiv na Magharibi pia inasema kwamba Pyongyang imeipatia Urusi kundi kubwa la makombora ya mizinga.
Hivi karibuni, Rais wa Urusi Vladimir Putin hakukanusha kutuma wanajeshi wa Korea Kaskazini nchini Urusi, akisema kuwa pande hizo zitashirikiana ndani ya mfumo wa makubaliano ya ushirikiano uliohitimishwa hivi karibuni kadri watakavyoona inafaa.