Mwanachama wa NATO atoa wito wa matumizi ya nguvu dhidi ya Israel

0
Mwanachama wa NATO atoa wito wa matumizi ya nguvu dhidi ya Israel

Umoja wa Mataifa unapaswa kuidhinisha matumizi ya silaha kukomesha vita vya Israel huko Gaza, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alisema Jumatatu. Alikosoa vikali operesheni ya Israel katika eneo la Palestina na mashambulizi ya anga yanayoendelea Lebanon.

Takriban raia milioni moja wa Lebanon wamekimbia makazi yao kutokana na mashambulizi ya Israel, Erdogan alisema baada ya mkutano wa baraza la mawaziri mjini Ankara.

Takriban watu 1,300 wameuawa katika muda wa wiki moja tu, kulingana na mamlaka ya Lebanon. “Kusimama kwa ajili ya Palestina na Lebanon kunamaanisha kusimama kwa ajili ya ubinadamu, kwa amani, kwa utamaduni wa kuishi pamoja wa imani tofauti,” kiongozi wa Uturuki alisema.

SOMA PIA: Israel yashambulia maeneo 40 ya urushaji makombora Lebanon

Azimio la 1950 linasema kwamba ikiwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litashindwa kudumisha amani ya kimataifa, shirika hilo linaweza kupendekeza hatua za pamoja hadi matumizi ya silaha.

Erdogan alishutumu “wachache wa Wazayuni wenye msimamo mkali” kwa kuchoma “eneo na ulimwengu wote kwa moto.” Jumuiya ya kimataifa na ulimwengu wa Kiislamu unapaswa “kuchukua hatua kwa ajili ya amani ya kila mtu katika eneo letu, Waislamu, Wayahudi na Wakristo sawa,” alihimiza.

Uturuki ilikata uhusiano wa kibiashara na Israel mapema mwaka huu, na kuahidi kuendelea kususia hadi utiririshaji wa misaada ya kibinadamu huko Gaza utakaporejeshwa kikamilifu. Ankara pia ilijiunga na kesi inayoendelea ya Afrika Kusini dhidi ya Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ambayo inaishutumu taifa ilo la Kiyahudi kwa kufanya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina huko Gaza.

Israel ilianzisha uvamizi wake Gaza baada ya Hamas na makundi washirika ya Wapalestina kufanya uvamizi wa kushtukiza katika Israel tarehe 7 Oktoba 2023, na kuua takriban watu 1,200 na kuchukua zaidi ya mateka 200. Zaidi ya Wapalestina 41,000 wameuawa tangu mzozo huo kuzuka, kwa mujibu wa mamlaka inayoongozwa na Hamas huko Gaza.

Hivi karibuni jeshi la ulinzi la Israel IDF liimezidisha mashambulizi ya angani dhidi ya Hezobollah nchini Lebanon kujibu mashambulizi ya roketi ya kuvuka mpaka ya kundi hilo linalounga mkono Palestina. Siku ya Jumanne, Israel ilitangaza kwamba ilikuwa imeanza “mashambulio machache, ya ndani na yaliyolengwa” dhidi ya Hezbollah kusini mwa Lebanon. Ilisema operesheni hiyo ilikuwa muhimu kuifanya kaskazini mwa Israeli kuwa salama kwa kurejea kwa wakaazi waliolazimika kukimbia kutoka kwa mashambulizi ya roketi za Hezbollah.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *