Mpango wa siri wa Israeli wa miaka 20 wa kuishambulia Iran: Silaha za hali ya juu zafichuliwa
Katika miongo ya hivi karibuni, taasisi ya ulinzi ya Israel imewekeza mabilioni ya fedha katika kutayarisha mashambulizi yanayoweza kutokea dhidi ya Iran, ikitengeneza silaha maalum katika kipindi cha miaka 20. Baadhi ya uwezo huu ulifichuliwa tu baada ya silaa izo kuuzwa kwa vikosi vya anga vya kigeni. Hapa kuna kile kinachoweza kufichuliwa kati ya maandalizi haya.
Mwezi uliopita, Israel ilifanya mashambulizi nchini Yemen, kwa kupeleka ndege za F-15 kutoka kituo kilicho umbali wa kilomita 1,800, kuonyesha ustadi na uboreshaji wa ndege hizi. Ndege hizi, zilizoundwa awali kwa ajili ya mapigano ya angani, zilirekebishwa nchini Israeli kwa misheni za mashambulizi. Jeshi la Wanahewa la Israeli pia liliwapa vifaa vya kubeba zana za kisasa kutoka kwa watengenezaji wa Amerika na Israeli.
Walakini, shambulio dhidi ya Irani linatoa changamoto ngumu zaidi, licha ya umbali sawa na shambulizo lile la Yemen.
Vifaa vya nyuklia vya Iran na kambi za makombora ya balestiki zimewekwa chini ya ardhi, tofauti na malengo ambayo hayalindwi kama vituo vya mafuta. Zaidi ya hayo, Iran inaendesha mfumo wa hali ya juu wa ulinzi wa anga, ambao kimsingi umeendelezwa ndani ya Iran yenyewe.
Kulingana na madai yao, ambayo bado hayajajaribiwa, mfumo huu unalingana na uwezo wa mifumo ya Urusi kama S-300, ambayo inaweza kuzuia makombora yaliyorushwa na Israeli. Walakini, shambulio lililohusishwa na Israeli huko Isfahan baada ya shambulio la Aprili la Iran halikuzuiliwa na ulinzi huu wa hali ya juu. Iran pia inadumisha ndege za kivita zilizopitwa na wakati, zikiwemo MiG-29 za Urusi na F-14 za Marekani, ambazo zinaendelea kufanya kazi licha ya vikwazo vya kimataifa.
Kwa kuzingatia changamoto hizo, vikosi vya ulinzi vya Israel vimetumia miaka 20 kujiandaa kwa uwezekano wa kuishambulia Iran, vikiwekeza mabilioni ya dola na shekeli. Uwekezaji huu unajumuisha kutengeneza silaha maalum, ambazo baadhi yake hata Marekani ilikataa kuiuzia Israel, pamoja na ubunifu ambao haupatikani kwa U.S.
Shambulizi kutoka umbali wa kilomita 1,800
Mashambulizi katika umbali wa kilomita 2,000 kwa kawaida hufanywa na vikosi vya Marekani na Urusi kwa kutumia makombora ya cruise na ndege za kubeba vilipuzi maarufu kama Bombers. Israel, hata hivyo, imetenga sehemu kubwa ya usaidizi wake wa Marekani kupata ndege za kivita zenye uwezo wa kuruka saa mbili kwenda na kurudi—kuanzia kikosi cha juu cha ndege za F-15I hadi vikosi vinne vya F-16I Sufa.
Lockheed Martin ambayo ni kampuni ya Marekani ambayo hutengeneza ndege na makombora ya kijeshi, ilitengeneza matangi ya mafuta yasiyo rasmi mahsusi kwa ajili ya jeti hizi, na kuimarisha anuwai zake bila kuathiri kwa kiasi kikubwa nguvu za anga au usahihi wa rada.
Ripoti za kigeni zinaonyesha kuwa Israel imetengeneza matangi ya mafuta yanayoweza kutengwa kwa ajili ya ndege za F-35, na kuziwezesha kufika Iran huku zikiwa na uwezo wa kutoonekana kwenye Rada.
Makombora ya Mashambulizi ya masafa marefu
Mwishoni mwa miaka ya 2000, viwanda vya ulinzi vya Israel vilifichua makombora mawili ya masafa marefu yaliyorushwa kutoka kwa ndege za kivita. Ingawa maelezo kama vile masafa mahususi hayajabainika, inajulikana kuwa yana safu ya mamia ya kilomita, ambayo yanaruhusu mashambulizi kutoka nje ya safu mbalimbali za ulinzi wa Irani.
Makombora haya husafiri kwa kasi ya ajabu, na hivyo kupunguza nyakati za tahadhari za adui na kutatiza juhudi za kuzuiwa, na kuongeza nafasi zao za kugonga shabaha.
Kombora la Rampage
Rampage, iliyotengenezwa kwa ushirikiano kati ya Israel Aerospace Industries (IAI) na Elbit Systems, inategemea roketi ya EXTRA ya Elbit. Hapo awali iliundwa kwa ajili ya uzinduzi wa ardhi, Rampage ilichukuliwa kwa ajili ya mashambulizi ya angani, na ilipewa uwezo mashambulizi kutoka kwenye Ndege za kivita ( jeti).
Ikiwa na urefu wa mita 4.7, kipenyo cha cm 30.6, na uzito wa kilo 570, kombora la Rampage hubeba kichwa cha kivita cha kilo 150, na kulifanya kuwa na ufanisi dhidi ya betri za kombora, vituo vya amri, na malengo mengine muhimu. Kombora hili linaweza pia kurushwa kutoka kwa ndege za Israel F-15, F-16, na F-35. Kuegemea kwake kwa teknolojia iliyopo ya roketi kunaifanya iwe nafuu, inakadiriwa kuwa dola laki chache kwa kila kitengo.
Rocks Missile
Kombora la Rocks Missile, lililozinduliwa na Rafael Advanced Defense Systems Ltd. ambayo ni kampuni ya teknolojia ya ulinzi ya Israeli mnamo 2019, linachanganya uwezo wa kusafiri wa ajabu na urambazaji wa satelaiti, pamoja na optical targeting. Linatokana na kombora la ‘Anchor’ la kampuni iyo ya Rafael, ambalo linaiga kombora la Shahab la Iran kwa kasi na uelekevu kwa madhumuni ya majaribio.
Rocks inaweza kuzinduliwa kutoka kwa ndege ndogo za F-16 na uwezekano wa F-35. Tathmini za kigeni zinaonyesha kuwa liina umbali wa kilomita 300 na linaweza kubeba kichwa cha kivita cha kilo 500, na kuifanya kuwa na uwezo wa kulenga miundo iliyoimarishwa au ya chini ya ardhi.
Maendeleo ya Ziada
Duru za kigeni zinaonyesha kuwa Israel ina mfumo wa makombora ya uso kwa uso, yenye vichwa vya kawaida na vya nyuklia, yanayojulikana kama makombora ya “Jericho”. Licha ya mamia ya makombora ya balestiki ambayo Iran imerusha kuelekea Israel, uwezekano wa Israel kutumia makombora hayo katika shambulizi unaonekana kuwa mdogo. Makombora haya yalitengenezwa hapo awali na kampuni ya Ufaransa ya Dassault, baadaye kuboreshwa na kampuni ya israel ya Israel Aerospace Industries (IAI).
Israel inashikilia sera ya utata kuhusu uwezo wake katika eneo hili, mara nyingi ikitangaza “majaribio ya urushaji wa roketi” wakati wa kurusha kutoka kituo chake cha Palmachim. Hata hivyo, uzinduzi wa 1988 wa mfumo wa kurusha setilaiti wa ‘Shavit’ ulithibitisha uwezo wa masafa marefu wa Israel wa balestiki, kwani kirusharusha satelaiti chochote kinaweza kubadilishwa kwa matumizi ya kijeshi.
Zaidi ya hayo, Kampuni ya Elbit imetengeneza mabomu ya kulipua mahandaki ya chini ya ardhi, yaliyopewa jina la 500MPR, yenye uwezo wa kupenya hadi mita 4 za ardhini. Mabomu haya, yaliyojaribiwa kwenye jeti za F-15I, yana masafa mafupi, yanayofikia kilomita kadhaa kulingana na njia ya kupelekwa.
PopEye Turbo
Silaha nyingine ya Israeli, inayojulikana tu kutokana na ripoti za kigeni, ni kombora la kusafiri la “PopEye Turbo”, lililotengenezwa na kampuni ya Rafael Advanced defence System kwa umbali wa kilomita 1,500.
Imeundwa ili kuzinduliwa kutoka kwa manowari za Jeshi la Wanamaji la Israeli na ina uwezo wa kubeba vichwa vya kawaida na vya nyuklia. Kombora hili huruhusu manowari za Israeli kushambulia Iran kutoka Bahari Nyekundu au Bahari ya Arabia bila kuingia Ghuba ya Uajemi.
Kusafirisha silaha hizi za hali ya juu kwa wateja wa kigeni wanaoaminika, huruhusu kampuni za Israeli kuwekeza tena katika utengenezaji wa makombora na mabomu, na hivyo kupunguza gharama kwa Wizara ya Ulinzi ya Israeli. Kuna uwezekano kwamba silaha ambazo hazijafichuliwa zimehifadhiwa katika maghala ya Jeshi la Wanahewa la Israeli, zikingojea wakati mwafaka.