Milipuko mipya imesikika Lebanon huku Israel ikiapa kushambulia benki za Hezbollah
Israel imefanya mashambulizi zaidi ya anga huko Beirut na kusini mwa Lebanon, ikiwa ni pamoja na matawi ya benki ambayo inasema inaunga mkono Hezbollah.
Milipuko ilisikika katika wilaya ya Dahieh ya Beirut kusini, eneo linalodhibitiwa na Hezbollah, pamoja na Bonde la Bekaa na kusini mwa Lebanon. Bado haijulikani ikiwa kuna majeruhi wowote.
Soma Pia: Mpango wa siri wa Israeli wa miaka 20 wa kuishambulia Iran: Silaha za hali ya juu zafichuliwa
Jeshi la Israel awali lilionya watu wanaoishi katika maeneo 25 nchini Lebanon – ikiwa ni pamoja na 14 katika mji mkuu Beirut – kwamba ilipanga kufanya mashambulizi usiku kucha.
Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) pia lilisema litalenga benki na miundombinu mingine ya kifedha inayosaidia Hezbollah.
Katika taarifa iliyotolewa Jumapili jioni, msemaji wa IDF Adm Daniel Hagari alionya kwamba “mtu yeyote aliye karibu na maeneo yanayotumiwa kufadhili shughuli za ugaidi za Hezbollah lazima aondoke kwenye maeneo haya mara moja”.
“Tutashambulia maeneo lengwa kadhaa katika saa zijazo na maeneo mengine lengwa zaidi usiku kucha,” alisema.
“Katika siku zijazo, tutafichua jinsi Iran inavyofadhili shughuli za kigaidi za Hezbollah kwa kutumia taasisi za kiraia, vyama na mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo yanatumika kama vyanzo vya pesa za ugaidi,” msemaji huyo wa Israel aliongeza.
Shirika la habari la serikali ya Lebanon NNA liliripoti mashambulizi kwenye matawi ya benki ya Al-Qard Al-Hassan association, ikiwa ni pamoja na Mashariki ya Bekaa Valley.
UCHAMBUZI KAMALIZI TAZAMA VIDEO HAPA CHINI
Tazama Video zaidi