Taliban yakataa ombi la Trump la kurejesha silaha za Marekani zenye thamani ya dola bilioni 7
Taliban yakataa ombi la Trump la kurejesha silaha za Marekani zenye thamani ya dola bilioni 7
Kundi la Taliban wamesisitiza kwamba wanahitaji silaha zaidi, ili kupigana na kundi la ISIS-K pamoja na Jimbo la Kiislamu – Mkoa wa Khorasan ambalo ni tawi la kikanda la kundi la wanajihadi la Salafi la Islamic State linalofanya kazi katika Asia ya Kusini-Kati, hasa Afghanistan na Pakistan, badala ya kurudisha silaha kwa Marekani.
Kundi hilo la Taliban nchini Afghanistan wanashikilia msimamo wao wa kutorudisha vifaa vya kijeshi ambavyo jeshi la Marekani liliacha wakati likiondoka katika taifa hilo la Asia Kusini mwaka 2021, iliripoti Bloomberg.
Akizungumza na vyombo vya habari, mtu ambaye hataki kutambuliwa, alisema kuwa Taliban walisisitiza kuwa wanahitaji silaha zaidi, risasi, silaha za kuendeleza kupigana na ISIS-K, Islamic State Khorasan badala ya kurejesha silaha hizo.
Jibu hili lilikuja baada ya matamshi ya Trump katika mkutano wa hadhara, ambapo aliitishia Afghanistan kwa kunyakua msaada wote wa kifedha ikiwa taifa hilo halitarudisha ndege za Marekani, silaha za anga hadi ardhini, magari na vifaa vya mawasiliano.
Trump alisema, “Ikiwa tutalipa mabilioni ya dola kwa mwaka, waambie hatutawapa pesa isipokuwa warudishe zana zetu za kijeshi.”
Walakini, msemaji wa Taliban hakujibu maoni yaliyotolewa na Rais wa Marekani Donald Trump.
Wanajeshi wa Marekani waliondoka Afghanistan baada ya kutumwa nchini humo kwa miaka 20. Jeshi hilo la Marekani liliacha silaha zenye thamani ya dola bilioni 7 na kuondoka nchini humo, baada ya kuzidiwa na Talibam.
Licha ya kukataa matakwa ya Trump, Taliban imetafuta mwanzo mpya na Marekani chini ya rais wake mpya, na kupata ufikiaji wa karibu dola bilioni 9 katika akiba ya fedha za kigeni iliyohifadhiwa.
Taliban inataka kuanzisha uhusiano wa amani na Marekani ili kufikia kutambuliwa kimataifa kwa serikali yake ya pariah (Isiyotambulika kimataifa), na fedha hizo zitatoa msaada kwa nchi hiyo iliyodhoofika kiuchumi ambayo imepoteza misaada ya kimataifa pia, ripoti hiyo ya Bloomberg iliongeza.
Siku ya Jumanne, utawala wa Taliban ulisema kuwa umebadilishana Mmarekani na Mfghanistan ambaye alifungwa katika jela ya Marekani.
Ingawa mataifa machache, kama vile China, Pakistan, na Urusi, yamewakaribisha mabalozi wa Taliban, hayatambui rasmi utawala huo, ambao umelaaniwa sana kwa ukiukaji wake mwingi wa haki za binadamu.
Mwaka jana, China ilikuwa nchi ya kwanza kutoa kitambulisho cha kidiplomasia cha Taliban.