Urusi yadungua Jeti tatu za Ukraine – Wizara ya Ulinzi ya Urusi

0
Urusi yadungua Jeti tatu za Ukraine

Vikosi vya Urusi vimedungua ndege tatu za kivita za Ukraine katika muda wa saa 24 zilizopita, Wizara ya Ulinzi mjini Moscow imesema.

Ndege mbili aina ya Sukhoi Su-27 zinazoendeshwa na Kiev ziliharibiwa na Vikosi vya Wanaanga vya Urusi, huku ulinzi wa anga wa Urusi ukiidungua ndege ya Mikoyan MiG-29, wizara ilisema katika chapisho lake la kila siku Jumapili.

Katika kipindi hicho, ulinzi wa anga wa Urusi pia ulinasa roketi iliyotengenezwa na Marekani  ya HIMARS, mabomu manne ya kuongozwa na Hammer yaliyotengenezwa na Ufaransa, na drones 55, iliongeza taarifa iyo.

Katika muda wa saa 24 zilizopita, vikosi vya Ukraine vilipoteza zaidi ya askari 2,200 kwenye mstari wa mbele na vitengo kadhaa vya vifaa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na vipande kadhaa vya silaha vya M777 vilivyotengenezwa na Marekani na ndege za L-119 za Uingereza.

Uzalishaji wa Su-27s na MiG-29s ulianza katika Umoja wa Kisovieti mapema miaka ya 1980, na ndege hizo za kivita zilikusudiwa kukabiliana na ndege za kizazi cha nne za Marekani kama vile F-15s na F-16s.

SOMA PIA: Putin atoa onyo jipya kwa NATO – Vita vya moja moja kwa NATO

Mnamo Julai, Jarida Forbes liliripoti, likinukuu data ya uchambuzi wa Oryx, kwamba Ukraine ilikuwa na ndege za kivita (jeti) 125 zikiwemo Su-27, Su-25s, MiG-29s na zingine wakati mzozo kati ya Moscow na Kiev ulipoongezeka mnamo Februari 2022. Takriban ndege 90 kati ya hizo zimeshambuliwa na kuharibiwa tangu wakati huo.

“Muungano” wa mataifa ya Ulaya, ikiwa ni pamoja na Uholanzi, Denmark, Norway na Ubelgiji, uliahidi kuipatia Kiev ndege 80 za F-16 zaidi ya mwaka mmoja uliopita.

Ukraine, ambayo ilikuwa imepokea chini ya ndege izo kumi na mbili zilizoundwa na Marekani mwanzoni mwa Agosti, ilipoteza ndege yake ya kwanza ya F-16 wakati ndege iyo ilipotumiwa mara kwenye vita mwishoni mwa mwezi wa nane. Ndege hiyo ya kivita ya nchi za Magharibi ilianguka wakati wa shambulizi la kombora la Urusi na ndege zisizo na rubani kwenye maeneo yaliyolengwa mjini Kiev, na kumuua mmoja wa marubani wenye uzoefu mkubwa nchini humo, Aleksey ‘Moonfish’ Mes.

Wachunguzi wa Ukraine bado hawajatangaza sababu za ajali hiyo. Lakini hata ivo wizara ya Ulinzi ya Urusi haikuripoti kudungua ndege iyo aina ya F-16. Baadhi ya vyombo vya habari vya Urusi vilidai kuwa ndege hiyo ya Magharibi ingeweza kua ilishambulwa na kombora la la ardhini la Iskander wakati wa shambulio kwenye uwanja wa ndege magharibi mwa Ukraine.

Mnamo Machi, Rais wa Urusi Vladimir Putin alisema kuwa matumizi ya F-16 katika mzozo huo yatakuwa “lengo halali” la vikosi vya Urusi, akionya kwamba ndege hizo zitapigwa hata kwenye viwanja vya ndege ndani ya nchi za NATO ikiwa zitafanya kazi kutoka huko.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *