Tanganzo la kuripoti shule ya Polisi Moshi 2024
Tanganzo la kuripoti shule ya Polisi Moshi 2024, Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga na Jeshi la Polisi 2024 | Tangazo La Kuripoti Shule Ya Polisi Moshi Kwa Vijana Waliochaguliwa Kujiunga Na Jeshi La Polisi Tanzania | Waliopata Kazi za Polisi September 2024
TANGAZO LA KURIPOTI SHULE YA POLISI MOSHI KWA VIJANA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI TANZANIA
1. Mkuu wa Jeshi la Polisi anawatangazia vijana wote waliochaguliwa kujiunga na Jeshi la Polisi Nchini kuwa wanatakiwa kuripoti Shule ya Polisi Moshi kuanzia tarehe 30/09/2024 hadi tarehe 02/10/2024 kwa ajili ya kuhudhuria mafunzo.
2. Vijana waliofanyiwa usaili Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam (DPA) na Vikosi vilivyo chini ya Makao Makuu ya Polisi wanatakiwa kuripoti Dar es salaam eneo la Polisi (Barracks) Barabara ya Kilwa karibu na Hospitali Kuu ya Polisi tarehe 30/09/2024 saa 12.00 asubuhi kwa ajili ya safari ya kwenda Shule ya Polisi Moshi.
3. Vijana waliofanyiwa usaili Mikoa ya Tanzania Bara wanatakiwa kuripoti kwa Makamanda wa Polisi wa Mikoa waliofanyia usaili tarehe 29/09/2024 saa 2.00 asubuhi kwa ajili ya kupewa utaratibu wa safari ya kwenda Shule ya Polisi Moshi.
4. Vilevile, vijana waliofanyia usaili Zanzibar (Unguja na Pemba) wanatakiwa waripoti Makao Makuu ya Polisi Zanzibar (Ziwani) tarehe 29/09/2024 kwa ajili ya kupangiwa utaratibu wa safari.
5. Aidha, vijana wote waliochaguliwa wanatakiwa waripoti Shule ya Polisi Moshi wakiwa na vifaa vifuatavyo:
i) Track suti (track suit) rangi ya bluu (blue) yenye ufito mweupe, fulana (t-shirt) nyeupe isiyo na maandishi, raba, soksi nyeusi, bukta mbili (2) za bluu (blue) kwa ajili ya michezo na mazoezi pamoja na sanduku la chuma (Tranka) la rangi ya blue.
ii) Chandarua cheupe cha duara na sio cha pembe nne, shuka za light blue jozi mbili (Shuka 4), blanket moja la kijivu lisilo na maua na sio duveti na pasi ya mkaa.
iii) Vifaa vya usafi: reki, jembe lenye mpini, panga, ndoo mbili ndogo na fagio la chelewa.
iv) Kadi ya bima ya Afya (NHIF) au fedha taslimu Tsh. 50,400/= kwa wasio na kadi za bima ya Afya.
v) Vyeti halisi vya taaluma (Original Academic Certificates), cheti halisi cha kuzaliwa, kadi ya NIDA au namba ya Utambulisho wa Taifa (NIDA), Nakala za kadi za NIDA au namba za Utambulisho wa Taifa (NIDA) za wazazi na watu wa karibu upande wa Baba na Mama (kama vile Baba Mkubwa, Mdogo, Shangazi, Mama mkubwa, mdogo, mjomba, Babu, Bibi nk) passport size 06 (background blue), na nakala (copy) 5 kwa kila cheti kilichoainishwa hapo juu.
vi) Fedha ya kujikimu.
6. Simu za mkononi haziruhusiwi chuoni, hivyo ni marufuku kuripoti Shule ya Polisi Moshi na simu ya mkononi. Yeyote atakaepatikana na simu itachukuliwa kuwa ni utovu wa nidhamu na adhabu yake ni kufukuzwa mafunzo mara moja. Shule itaelekeza utaratibu wa kupata mawasiliano.
7. Kwa yeyote atakaye ripoti Shule ya Polisi Moshi baada ya tarehe 02/10/2024 hatopokelewa na atahesabika amejiondoa mwenyewe kwenye mafunzo.
8. Orodha ya vijana waliochaguliwa imeambatishwa kwenye tangazo hili