TAARIFA MUHIMU KWA WANAFUNZI WA STASHAHADA (DIPLOMA) – HESLB
TAARIFA MUHIMU KWA WANAFUNZI WA STASHAHADA (DIPLOMA)
1. Kuanzia mwaka wa masomo 2023/2024 Serikali ilianza kutoa mikopo kwa wanafunzi wenye sifa nzuri za stashahada (Diploma) za kipaumbele kwa Taifa ambazo zinatajwa kwa kina katika ‘Mwongozo wa Utoaji Mikopo kwa Stashahada kwa 2024/2025’ unaopatikana katika http://heslb .go.tz;
2. Hivyo, katika mwaka wa masomo 2024/2025 unaotarajiwa kuanza mwezi Oktoba, 2024, wanafunzi wenye sifa wanaendelea kuomba ili hatimaye kuwezeshwa kusoma kozi za stashahada;
3. Kwakuwa dirisha la kuomba mikopo kwa njia ya mtandao linakaribia kufungwa, (Agosti 31, 2024) tunawakumbusha kuwa stashahada zinazopewa kipaumbele katika maeneo ya kuweka:
a. Afya na Sayansi Shirikishi
b. Elimu na Mafunzo ya Ufundi
c. Usafiri na Lojistiki
d. Uhandisi wa Nishati, Madini na Sayansi ya Ardhi
e. Kilimo na Mifugo
f. Kozi nyinginezo
‘Energy Engineering’, ‘Mining & Earth Science’, na ‘Agriculture & Livestock’ ambazo hazikutajwa kwenye kipengele cha D na E kama tangazo linavyoonesha, wanaruhusiwa kuomba mkopo na watapimwa uhitaji wao wa mkopo kupitia kingámua uwezo.
KUMBUKA: Ili kuomba mkopo, tembelea: https://olas.heslb.go.tz/olams/pre-applicant
Imetolewa na:
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu
Jumatano, Agosti 28, 2024