Papa awaambia Wakatoliki wa Marekani kuchagua kati ya mwenye uovu mdogo au mkubwa (Trump na Kamala)

0
Papa awaambia Wakatoliki wa Marekani kuchagua kati ya mwenye uovu mdogo au mkubwa (Trump na Kamala)

Papa Francis aliwaambia waandishi wa habari siku ya Ijumaa kwamba, Wagombea urais wa Marekani Donald Trump na Kamala Harris wote “wanapingana na haki ya mtu kuishi,” na wapiga kura Wakatoliki wa Marekani wanapaswa kuchagua “mgombea ambae ni muovu mdogo,”

Akizungumza na waandishi wa habari alipokuwa akirejea Roma kutoka Singapore, papa huyo alisema kwamba “kutopiga kura ni jambo gumu,” na kwamba waumini “lazima wapige kura.”

“Lazima uchague uovu mdogo,” Papa alifafanua. “Ni nani mbaya zaidi? Yule bibi, au yule bwana? sijui. Ikiwa ni yule anayefukuza wahamiaji, au yule anayeua watoto, wote wawili wanaenda na kinyume cha maisha.”

SOMA PIA: Kuwazuia wahamiaji kuingia Ulaya ni ‘dhambi kubwa’ – Papa Francis

Iwapo atachaguliwa, Trump ameahidi kufunga mpaka wa kusini wa Marekani na kuongoza “operesheni kubwa zaidi ya kuwafukuza katika historia ya Marekani.” Harris ameapa kutia saini sheria inayohakikisha upatikanaji sawa wa utoaji mimba kama ilivyokuwa chini ya Roe v. Wade, uamuzi wa kihistoria wa Mahakama ya Juu ambao ulibatilishwa mwaka wa 2022.

Kuwafukuza wahamiaji, … ni jambo baya, kuna uovu huko. Kutoa mtoto kutoka tumboni mwa mama ni mauaji, kwa sababu kuna maisha. Ni lazima tuzungumze kuhusu mambo haya kwa uwazi,” Papa Francis aliwaambia wanahabari siku ya Ijumaa.

Papa amekuwa akipinga utoaji mimba, kulingana na mafundisho ya Kikatoliki. Hata hivyo, amewaruhusu makasisi kusamehe utoaji mimba, na kuwataka maaskofu kutokataa ushirika kwa wanasiasa wanaounga mkono mila hiyo.

Pia amechukua msimamo huria zaidi katika masuala yanayohusiana na uhamiaji kuliko watangulizi wake. Wakati wa uchaguzi wa urais wa 2016, alikosoa pendekezo la Trump la kuweka ukuta kwenye mpaka wa Marekani/Mexico na kumtaja Trump kama “sio Mkristo,” na mwaka wa 2019 Vatikani ilitoa $500,000 kwa wahamiaji 75,000 wa Amerika ya Kati wanaojaribu kufika Marekani kupitia Mexico.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *