Putin atoa onyo jipya kwa NATO – Vita vya moja moja kwa NATO

0
Putin atoa onyo jipya kwa NATO

Putin atoa onyo jipya kwa NATO

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameonya kuwa, Kuondoa vikwazo vya matumizi ya silaha za nchi za Magharibi kwa Ukraine kutahusisha moja kwa moja Marekani na washirika wake katika mzozo na Urusi na akaonya kwamba kutapatiwa jibu mwafaka kutoka kwa Urusi.

Nchi za Magharibi zimeitumia Ukraine makombora ya masafa marefu kama vile Storm Shadows na ATACMS, ambayo hadi sasa Kiev imetumia dhidi ya Crimea na Donbass. Hata hivyo, Katika siku kadhaa zilizopita, Marekani na Uingereza zimependekeza kuwa zinaweza kuruhusu silaha hizi kutumika kulenga shabaha ndani zaidi ya ardhi ya Urusi inayotambulika kimataifa.

“Hatuzungumzii juu ya kuruhusu au kuzuia serikali ya Kiev kushambulia eneo la Urusi,” bali Ukraine tayari Inafanya hivyo kwa kutumia ndege sizizo na rubani na njia zingine.” Putin alisema Alhamisi.

Ukraine haina uwezo wa kutumia mifumo ya masafa marefu ya nchi za Magharibi, Putin aliongeza, akibainisha kuwa kulenga mashambulizi kama hayo kunahitaji taarifa za kijasusi kutoka kwa satelaiti za NATO, kwaiyo suluhu ya kutumia mifumo iyo ya masafa marefu inaweza kufanywa ivo na wanajeshi wa NATO.”

“Iwapo uamuzi huu utafanywa, haitakuwa na maana zaidi ya ushiriki wa moja kwa moja wa nchi za NATO, Marekani na nchi za Ulaya, katika mzozo wa Ukraine,” rais wa Urusi alisema. “Ushiriki wao wa moja kwa moja, bila shaka, unabadilisha kwa kiasi kikubwa kiini, asili ya mzozo.”

Kwa kuzingatia hilo, Putin aliongeza, Urusi “itafanya maamuzi yanayofaa kulingana na vitisho vinavyotukabili.”

SOMA PIA: Zelensky akataa ‘mipango ya amani’ ya Brazil na China

Baadhi ya vikwazo vya matumizi ya silaha zinazotolewa na nchi za Magharibi viliwekwa awali ili kuruhusu Marekani na washirika wake kudai kuwa hawakuhusika moja kwa moja katika mzozo na Urusi, huku wakiipa Ukraine silaha za dola bilioni 200. Kiev imekuwa ikipiga kelele kutaka vikwazo viondolewe tangu Mei.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza David Lammy wamedokeza kwamba vikwazo hivyo huenda vikaondolewa wiki hii, wakitaja madai ya kuwasilishwa kwa makombora ya balistiki ya Iran kwenda Urusi kama kisingizio. Iran imekanusha kutuma makombora yoyote kwa Urusi, ikiziita tuhuma hizo “vita vya kisaikolojia” na nchi zinazohusika pakubwa katika kuipatia silaha Ukraine.

Putin hapo awali aliwaonya wanachama wa NATO kufahamu “wanachocheza nacho” wakati wa kujadili mipango ya kuruhusu Kiev kushambulia ndani ya ardhi ya Urusi kwa kutumia silaha zinazotolewa na Magharibi.

Akizungumza na mashirika makubwa ya habari kando ya Kongamano la Kimataifa la Kiuchumi la St.Petersburg mwezi June, rais wa Urusi alisema Urusi itajibu kwa kudungua silaha zinazohusika na kisha kulipiza kisasi dhidi ya waliohusika.

Moja ya majibu yanayowezekana ambayo Putin alitaja wakati huo ni kuwashambulia maadui wa nchi za Magharibi kwa silaha za masafa marefu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *