Majina ya Wanafunzi na Shule Walizopangiwa Kidato cha Kwanza 2025
Majina ya Wanafunzi na Shule Walizopangiwa Kidato cha Kwanza 2025 | Shule walizopangiwa form one 2025 (Shule walizopangiwa kidato cha kwanza 2025) | Uchaguzi wa Kidato cha Kwanza 2025 | Shule walizopangiwa Darasa la saba
Kila mwaka, mamilioni ya wanafunzi nchini Tanzania huhitimu masomo yao ya elimu ya shule ya msingi na kujiandaa kwa hatua inayofuata: kujiunga na shule za sekondari. Uchaguzi wa kidato cha kwanza ni tukio muhimu linaloamua mustakabali wa mwanafunzi. Mwaka huu wa 2025, Serikali ya Tanzania, kupitia Tamisemi, inatarajiwa kutangaza matokeo ya uchaguzi wa kidato cha kwanza.
Mchakato wa uchaguzi wa kidato cha kwanza 2025 ni muhimu sana kwani unaamua shule gani mwanafunzi atajiunga nayo. Shule za sekondari hutofautiana kwa ubora wa walimu, vifaa vya kufundishia, na mazingira ya masomo. Kwa hiyo, uchaguzi sahihi wa shule unaweza kuwa na athari kubwa kwenye mafanikio ya mwanafunzi katika ngazi ya elimu ya sekondari.
WANAFUNZI WENYE UFAULU KATI YA 121 – 300 WOTE WAMEPANGIWA SHULE
Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kujiunga na Kidato cha Kwanza mwaka, 2025 umezingatia kigezo cha ufaulu wa mtahiniwa anayechaguliwa. Kila mtahiniwa aliyefanya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi mwaka, 2024 na kupata jumla ya alama za ufaulu kati ya 121 hadi 300 amechaguliwa na kupangiwa Shule ya Sekondari ya Serikali.
Uchaguzi huu umehusisha wanafunzi 974,332 sawa na asilimia 100 ya wanafunzi wote waliokuwa na sifa ya kuchaguliwa wakiwemo Wasichana 525,225 na Wavulana 449,107. Wanafunzi hao ni wale waliofanya na kufaulu Mtihani wa Kuhitimu Elimu ya Msingi mwaka, 2024.
WANAFUNZI WALIOFAULU WAMEPANGIWA SHULE ZA BWENI NA KUTWA
Shule za Sekondari za Serikali walizopangiwa wanafunzi zipo katika makundi mawili ambayo ni Shule za Bweni na Shule za Kutwa.
Shule za Sekondari za Bweni za Serikali zimegawanyika katika makundi matatu ambayo ni; Shule za Sekondari za Bweni za Wanafunzi wenye ufaulu wa Juu (Special@Schools), Shule za Amali za Kihandisi (Ufundi) na Bweni Taifa.
Shule za Bweni ni za Kitaifa hivyo, zimepangiwa Wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali ya nchi kwa kuzingatia mgawanyo wa nafasi uliobainishwa na vigezo vilivyowekwa ili kuimarisha Utaifa.
Majina ya Wanafunzi na Shule Walizopangiwa Kidato cha Kwanza 2025
CHAGUA MKOA ULIKOSOMA
ARUSHA | DAR ES SALAAM | DODOMA |
GEITA | IRINGA | KAGERA |
KATAVI | KIGOMA | KILIMANJARO |
LINDI | MANYARA | MARA |
MBEYA | MOROGORO | MTWARA |
MWANZA | NJOMBE | PWANI |
RUKWA | RUVUMA | SHINYANGA |
SIMIYU | SINGIDA | SONGWE |
TABORA | TANGA |