Chalamila ataka vijana wafundushwe maadili waache kutukana mtandaoni

Chalamila ataka vijana wafundushwe maadili waache kutukana mtandaoni

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila amesema anajiandaa kuwasilisha pendekezo maalum kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Ptof. Adolf Mkenda akitaka kuimarishwa kwa mafunzo ya maadili kwa Vijana ili kupunguza tabia ya kutukana mitandaoni.

Chalamila ametoa kauli hiyo leo Juni 15, 2026 alipokuwa akizungumza na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dar es salaam. Amesema Vijana wengi wanaotumia lugha zisizofaa kwenye mitandao ya Kijamii wanakosa malezi na mafunzo yanayohusu heshima, maadili pamoja na umuhimu wa baraka kutoka kwa Wazazi na Viongozi wa Jamii.

“Ndugu zangu Viongozi wa dini, najiandaa kupeleka proposal kwa Waziri wa Elimu, leo Vijana wengi wanatukana mitandaoni kwa sababu somo la laana na baraka hawajalipata,” alisema Chalamila. Katika maelezo yake, alitolea mfano simulizi za Biblia kuhusu Yakobo na Esau, akisisitiza umuhimu wa kuheshimu Maadili, Wazazi na Viongozi kama sehemu ya malezi yanayoweza kusaidia kujenga Jamii yenye nidhamu na heshima.

Image with Link Description of Image