Israeli ilishambuliwa kwa makombora ya hypersonic ya Iran

Israeli ilishambuliwa kwa makombora ya hypersonic ya Iran

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetangaza kuwa Iran ilitumia makombora ya Hypersonic kwa mara ya kwanza wakati wa mashambulizi yake dhidi ya Israel apo jana.

Iran ilirusha makombora kadhaa katika kile IRGC ilichokiita jibu la mauaji ya hivi karibuni ya Israel ya wakuu wa Hamas na Hezbollah, pamoja na jenerali wa Iran aliyekuwa Lebanon.

Image with Link Description of Image

Makombora ya Fattah-2 hypersonic yalitumiwa katika shambulio hilo na yalivuka rada za Israeli, vyombo vya habari vya Irani viliripoti Jumanne jioni, vikinukuu IRGC.

Jishi ilo la walinzi la Iran lilidai kuwa 80-90% ya makombora yaliyotumiwa katika ‘Operesheni hiyo yalipiga shabaha zilizolengwa, kati ya hizo ni kituo cha anga cha Tel Nof karibu na Tel Aviv na eneo la Netsarim karibu na Gaza, ambapo walisema “idadi kubwa ya mizinga ya Israel” iliharibiwa.

Iran pia ilidai kuziarubu idadi kadhaa ya ndege za kivita za F-35 za Israel katika kambi ya anga ya Nevatim, iliyoko katikati ya Beersheba na Bahari ya Chumvi.

Kwa upande wake jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) lilikadiria idadi ya makombora yaliyorushwa na Iran kuwa ni 180 na kukiri kwamba “mapigo machache” yalirekodiwa ndani ya eneo la Israel. Kulingana na IDF, makombora mengi yalizuiliwa kwa mafanikio. Mtu pekee aliyeripotiwa kupoteza maisha katika eneo hilo ni Mpalestina, ambaye inasemekana aliuawa na kipande cha kombora kilichoanguka karibu na Yeriko katika Ukingo wa Magharibi.

Shambulio la Jumanne lilikuwa kubwa zaidi kwa ukubwa na wigo kuliko shambulio la Aprili, ambalo shambulio la kwanza kabisa kama hilo kufanywa na Iran, ambapo makombora mengi ya balestiki na ndege zisizo na rubani zilirushwa dhidi ya Israeli kwa kulipiza kisasi kufuatia shambulio la anga kwenye ubalozi mdogo wa Irani huko Damascus.

Makombora ya hypersonic huruka popote kwa kasi mara tano hadi 25 ya kasi ya sauti. Iran ilizindua kombora lake la kwanza kama hilo, Fattah-1, Juni mwaka jana. Toleo la Fattah-2 lilioneshwa kwa umma mnamo Novemba. Makombora yote mawili hayakuwa yametumiwa kwenye vita.

SOMA PIA: Iran ilivorusha safu ya makombora dhidi ya Israel (VIDEOS)

Kwa mujibu wa Tehran, shambulio hilo la makombora lilikuwa ni jibu la mauaji ya Ismail Haniyeh, kiongozi wa kisiasa wa kundi la wapiganaji wa Palestina Hamas, ambaye aliuawa mjini Tehran mwezi Julai. Iran pia ilitaja mauaji ya kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah na Meja Jenerali wa IRGC Abbas Nilferoshan nchini Lebanon wiki iliyopita.

Israel imeapa kujibu mashambulizi, huku Iran ikionya kwamba mashambulizi yoyote zaidi yatakabiliwa kwa nguvu.