Kanisa la St Anne Buffalo Marekani lafungwa na kuuzwa kwa jumuiya ya Kiislamu kwa $250,000 ambao watageuza kanisa ili kuwa msikiti wa kihistoria

0

Dayosisi ya Kanisa Kikatoliki la Buffalo, huko New York Nchini Marekani imetoa maoni yake kuhusu kuuzwa kwa kanisa la kihistoria kwa jamii ya Waislamu wa eneo hilo, baada ya chapisho la mtandao wa kijamii kuhusu mpango huo kuzua maneno ya hasira.

Kanisa la Mtakatifu Anna lilijengwa mwaka wa 1886. Lilifungwa mwaka wa 2007, kwa kuwa hapakuwa na waumini wa kutosha kuliendeleza, na kuuzwa kwa kampuni moja mnamo 2022. Mapema mwezi huu, hata hivyo, lilitajwa kuwa mfano wa kupungua kwa Ukristo nchini Marekani.

“Kanisa linauzwa kwa jumuiya ya Kiislamu kwa $250,000 ambao wanageuza kanisa hilo la kihistoria kuwa msikiti,” akaunti inayoitwa ‘Father R. Vierling’ ilichapishwa kwenye X, ikiwa na picha za kanisa  kuu la mtindo wa Gothic. Chapisho hilo lilitazamwa mara milioni 11.

Baadhi ya maoni kwenye chapisho hilo yalikuwa ya hasira sana ambapo mtoa post alililazimika kujibu, Alikiwataka watu kutoelekeza hasira zao dhidi ya jamii ya Kiislamu. Alilaumu kuangamia kwa parokia hiyo kutokana na “kubadilika kwa idadi ya watu wa eneo hilo na kutokuwa na uwezo wa kifedha kwa kuendeleza kanisa hilo,” akibainisha kuwa “hali hii inatokea katika dayosisi kubwa za mijini nchini kote Marekani.”

Wasiwasi wa kifedha ndio ulikuwa sababu ya kuuzwa kwa Kanisa hilo, Dayosisi ya Buffalo iliimbia The Tablet, kituo cha Kikatoliki huko New York City. Kukarabati kanisa kungegharimu zaidi ya dola milioni 30 wakati huo, msemaji wa dayosisi Joe Martone alisema.

“Ilihitaji kiasi kikubwa cha pesa katika ukarabati,” Martone alisema. “Kazi iliyohitajika ilikuwa ghali sana na zaidi ya upeo wa dayosisi.”

Dayosisi ya Buffalo ilitangaza kufilisika mnamo 2020, chini ya mzigo wa tuhuma 900 za unyanyasaji wa kijinsia zilizohusisha makasisi na wafanyikazi wengine wa kikatoliki.

Mnamo Novemba 2022, dayosisi hiyo liliuza jumba lililofungiwa la St. Ann, pamoja na shule na jumba la watawa, kwa Buffalo Crescent Holdings. Wakati vyombo vya habari vya ndani viliripoti kwamba kampuni hiyo ilikusudia kubadilisha jengo hilo kuwa msikiti au kituo cha kiislam

Zaidi ya hayo, Martone alisema kuwa dayosisi hiyo ilikuwa imeachilia mali hiyo kwa “ajili ya matumizi mengine – profane use – neno linalorejelea makanisa yaliyofungwa ambayo hayatumiki tena kama makanisa, na kuyaruhusu kutumikia kusudi lolote mradi tu si “kufuru, ukosefu wa maadili, au kashfa.”

“Tumekuwa na mali zingine ambazo tumeuza ndani ya dayosisi ambazo zimeuzwa kwa vikundi vingine vya kidini ambavyo vimezitumia kwa huduma zao za kidini, kwa hivyo kwa ujumla, dayosisi haina shida na hilo,” aliongeza.

Buffalo ni jumuiya ya karibu watu 280,000 kwenye pwani ya Ziwa Erie, karibu na mpaka wa Marekani na Kanada. Tangu mwaka 2000, imeshuhudia wimbi la wahamiaji kutoka Yemen, Somalia, Bangladesh na Iraq.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *