Rais Putin atia saini amri mpya inayowaruhusu wageni kutafuta makazi ya muda nchini Urusi

Rais Putin atia saini amri mpya inayowaruhusu wageni kutafuta makazi ya muda nchini Urusi.

Putin anasema wale wanaotoroka kutoka kwa sera za “kiharibifu za uliberali mamboleo” za Magharibi za nchi zao, na kuwaalika kufuata maadili ya “kijadi” ya Urusi.

BONYEZA HAPA

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirika la habari la TASS la Urusi, inasema kwamba, Moscow itatoa msaada kwa wageni wowote ambao wanataka kutoroka maadili ya uliberali mamboleo yanayowekwa katika nchi zao na kuhamia Urusi, ambapo maadili ya kitamaduni yanatawala, kulingana na amri iliyotiwa saini na Rais Vladimir Putin.