TANGAZO LA FURSA 800 ZA AJIRA YA UDEREVA NCHINI QATAR

TANGAZO LA FURSA 800 ZA AJIRA YA UDEREVA NCHINI QATAR
TANGAZO LA FURSA 800 ZA AJIRA YA UDEREVA NCHINI QATAR
Image with Link Description of Image

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA WAZIRI MKUU

KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU

Image with Link Description of Image

TAARIFA KWA UMMA

TANGAZO LA FURSA 800 ZA AJIRA YA UDEREVA NCHINI QATAR

Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kwa Kushirikiana na kampuni tanzu ya Mkapa Foundation Imara Horizon, “Connect General Supplies Co. Ltd”, “Sassy Solutions Co. Ltd” pamoja na “Larali Global Solutions” inawatangazia Watanzania wenye sifa kutuma maombi kwa ajili ya kujaza nafasi 800 za fursa za udereva zilizotangazwa na kampuni ya MOWASALAT ya nchini Qatar kama ilivyoelezwa katika jedwali hapa chini: –

MAELEZO YA FURSA

  • Fursa: Dereva

  • Kampuni: Mowasalat

  • Nchi: Qatar

  • Umri: Miaka 25 – 45

Sifa Mwombaji:

  • Awe na elimu ya kidato cha Nne na kuendelea;

  • Awe na uzoefu wa zaidi ya miaka 2 katika fani ya Udereva;

  • Awe na uwezo wa kuzungumza lugha ya Kiingereza;

  • Mwenye uelewa na lugha ya Kiarabu atapewa kipaumbele.

Mambo muhimu

  • Mshahara utalipwa kulingana na Sera ya kampuni pamoja na sheria za nchi ya Qatar;

  • Gharama za matibabu kwa kipindi chote cha ajira zitakuwa juu ya muajiri;

  • Mwajiri atagharamia visa na tiketi ya ndege;

  • Mwajiri atagharamia malazi na chakula katika kipindi chote cha ajira;

Aina ya Ajira: Mkataba

Daraja la Leseni: Daraja C au E

Mwisho wa Kupokea maombi: 16 Mei, 2025

Jinsi ya kutuma maombi

Baada ya kutuma maombi unapaswa kujisajili https://jobs.kazi.go.tz

Simu Na. +255784301987

Tangazo hili limetolewa na:

KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI

OFISI YA WAZIRI MKUU

KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU