Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Mnyika amesema chama hicho kimepata hasara ya shilingi milioni 918 kutokana na kesi ya mgawanyo wa rasilimali.
Mnyika ameyasema hayo leo Juni 15, 2026 katika viunga vya Mahakama Kuu ya Tanzania, Masijala Ndogo ya Dar es salaam baada ya kuahirishwa kwa kesi nyingine ya mgawanyo wa rasilimali ndani ya chama hicho.
“Sisi CHADEMA tulikuwa na ushirikiano na chama cha nje na tulikuwa na mradi wa muda mrefu kidogo wa kujenga uwezo kwa Wanawake katika maeneo mbalimbali ya Nchi na masuala ya jinsia na mradi huu ulikuwa unatekelezwa na Tanzania Bara na Zanzibar, kipindi ambacho tumekewe zuio ni kipindi ambacho tulikuwa tunaendelea na mradi na kwa mkataba tuliokuwa nao hata wakati wa zuio walikuwa bado wanaingiza fedha kwenye akaunti”
“Ilipofika mwezi Disemba fedha ambazo ukizigeuza kwa fedha za Tanzania, jumla ni milioni 918 zuio lilipoondolewa muda wa kutekelezwa mradi ulikuwa umeshakwisha tumeambiwa turudisha fedha zile, sio hasara kwa CHADEMA bali ni Tanzania nzima ikiwa ni hasara za kifedha, kimali na kisiasa,”amesema Mnyika.





Leave a Reply
View Comments