Israel Yaendelea na Mashambulizi ya Anga Gaza Baada ya Mazungumzo na Hamas Kuvunjika

Israel Yaendelea na Mashambulizi ya Anga Gaza Baada ya Mazungumzo na Hamas Kuvunjika

Israel Yaendelea na Mashambulizi ya Anga Gaza Baada ya Mazungumzo na Hamas Kuvunjika

Israel imeanzisha tena mashambulizi ya anga katika Ukanda wa Gaza baada ya kushindwa kufikia makubaliano na Hamas kuhusu kuachiliwa kwa mateka waliobaki na utekelezaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano.

Image with Link Description of Image

Katika taarifa iliyotolewa mapema Jumanne, Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) lilisema kuwa linafanya mashambulizi makubwa dhidi ya malengo ya ugaidi ya Hamas ndani ya Ukanda wa Gaza.

Ofisi ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu ilisema kuwa mashambulizi hayo ni jibu kwa Hamas kukataa mara kwa mara kuwaachilia mateka, pamoja na kukataa mapendekezo yote yaliyowasilishwa na Mjumbe wa Rais wa Marekani, Steve Witkoff, na wapatanishi wengine.

“Kuanzia sasa, Israel itachukua hatua dhidi ya Hamas kwa nguvu kubwa zaidi za kijeshi,” ilisema ofisi ya Waziri Mkuu.

Kwa mujibu wa Al Jazeera, ikinukuu mamlaka katika Gaza inayoongozwa na Hamas, zaidi ya watu 200 wameuawatangu mapigano kuanza upya. Shirika la habari la Palestina, Wafa, liliripoti mashambulizi katikati na kusini mwa eneo hilo lenye msongamano mkubwa wa watu.


 

Hamas Yaishutumu Israel kwa Kuvunja Makubaliano ya Kusitisha Mapigano

Shirika la habari la Reuters lilimnukuu afisa wa ngazi ya juu wa Hamas akisema kuwa Israel imevunja kwa upande mmoja mkataba wa kusitisha mapigano, ambao ulidhaminiwa na Marekani na mataifa ya Kiarabu.

Kwa mujibu wa makubaliano yaliyoanza kutekelezwa Januari 19, Hamas iliwachilia mateka 25 na miili ya mateka wanane kwa kubadilishana na wafungwa wa Kipalestina 1,500 kutoka magereza ya Israel, kulingana na ripoti ya shirika la habari la AP.

Hata hivyo, Israel na Hamas wameshindwa kufikia makubaliano ya hatua zinazofuata tangu awamu ya kwanza ya makubaliano kumalizika Machi 1. Serikali ya Israel iliishutumu Hamas kwa kutumia hila na vita vya kisaikolojia, ikisema kuwa kundi hilo ndilo limekataa mpango wa hivi karibuni uliowasilishwa na mjumbe wa Marekani, Steve Witkoff.

Msemaji wa Hamas, Abdel-Latif Al-Qanoua, aliliambia Reuters mapema mwezi huu kwamba kundi hilo linashirikiana na wapatanishi kuishinikiza Israel kutekeleza awamu inayofuata ya makubaliano ya kusitisha mapigano.