Marekani yatishia Israel: Tatua mzozo wa kibinadamu huko Gaza au ukabiliane na vikwazo vya silaha – ripoti
Marekani imeamibia Israel kwamba itawekea vikwazo vya silaha kwa taifa hilo la Kiyahudi ikiwa haitasuluhisha mzozo wa kibinadamu huko Gaza, N12 iliripoti Jumanne.
Ikulu ya White House iliripotiwa kuelezea wasiwasi wake mkubwa juu ya “kuzorota kwa hali ya kibinadamu huko Gaza katika wiki za hivi karibuni” na kutoa wito wa hatua za haraka ndani ya mwezi ujao ili kubadili hali hiyo.
Waziri wa Masuala ya Kimkakati Ron Dermer na Waziri wa Ulinzi wa israel Yoav Gallant walipokea barua kutoka kwa Utawala wa Biden inayoelezea misimamo ya Marekani juu ya Gaza, N12 ilibaini.
Barua hiyo inaripotiwa kutaka Israel ishikilie ahadi yake ya Machi 2024 “kuruhusu na kutozuia uhamishaji wa misaada ya kibinadamu ya Marekani au misaada inayoungwa mkono na utawala huko Gaza.”
Kama sehemu ya ahadi hii, Idara ya Serikali “itafanya ukaguzi kwa mujibu wa sheria ya misaada.”
Barua hiyo inaripotiwa kuangazia kuwa tangu mwezi Machi, kiwango cha chini zaidi cha misaada kuingia Gaza kilirekodiwa mwezi Septemba.
Ripoti ya N12 Imeongeza kuwa Israel ilikuwa na siku 30 za kurekebisha hali hiyo na kwamba kutofanya hivyo kutasababisha madhara kwa misaada ya Israel, kwa mujibu wa sheria za Marekani.
Tangazo hilo lilitolewa muda mfupi baada ya Marekani kuamua kupeleka mfumo wake wa ulinzi wa makombora wa THAAD nchini Israel.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron pia ametoa wito wa kuwekewa vikwazo vya silaha Israel.