Matokeo ya Kidato cha sita (Form six) 2024 Haya hapa
Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha sita uliofanyika May mwaka huu 2024 ambapo jumla ya Watahiniwa 111,056 wa Shule na kujitegemea sawa na 99.43% ya Watahiniwa wenye matokeo ya mtihani huo wamefaulu.
Akitangaza matokeo hayo leo July 13,2024 Visiwani Zanzibar, Katibu Mtendaji wa NECTA, Dr. Said Mohamed, amesema “Wanawake waliofaulu ni 49,837 sawa na 99.61% wakati Wanaume waliofaulu ni 61,219 sawa na 99.28%, mwaka 2023 Watahiniwa waliofaulu walikuwa ni 104,549 sawa na 99.23%, hivyo ufaulu wa jumla umeongezeka kwa 0.20% ikilinganishwa na mwaka 2023”
“Watahiniwa wa Shule waliofaulu ni 103,252 sawa na 99.92% ya Watahiniwa wenye matokeo, Wanawake waliofaulu ni 46,615 sawa na 99.93% na Wanaume ni 56,637 sawa na 99.91%, Watahiniwa walioshindwa mtihani ni 84 sawa na 0.08%, mwaka 2023 watahiniwa 96,010 sawa na asilimia 99.90 ya
Watahiniwa wa Shule walifaulu mtihani huo, hivyo ufaulu wa Watahiniwa wa Shule umeongezeka kwa 0.02% ikilinganishwa na mwaka 2023”
“Idadi ya Watahiniwa wa kujitegemea waliofaulu mtihani ni 7,804 sawa na 93.34%, mwaka 2023 Watahiniwa wa kujitegemea 8,539 sawa na 92.30% walifaulu mtihani huo, hivyo ufaulu wa Watahiniwa wa kujitegemea umeongezeka kwa 1.04% ikilinganishwa na mwaka 2023”
- > MATOKEO YA KIDATO CHA SITA HAYA HAPA
- >MATOKEO YA MTIHANI WA UALIMU (DSEE) 2024
- >MATOKEO YA MTIHANI WA UALIMU (GATCE) 2024