Spika wa Bunge amuonya Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu Ado

Spika wa Bunge amuonya Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu Ado

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Zungu amemuonya Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu Ado @adoshaibuado kwa kitendo chake cha kuendelea kuzungumza baada ya Mwenyekiti wa Bunge kumjulisha kuwa muda wake umeisha na kuzimiwa kipaza sauti.

Spika amemuonya pia Ado kwa kitendo chake cha kurejea Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) ya Mwaka wa Fedha 2023/2024 kwa sababu bado haijafanyiwa kazi na Bunge kupitia Kamati za Bunge za PAC na LAAC ambayo Ado ndio Mwenyekiti wake.

Akichangia kwenye Hotuba ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ado Shaibu alizungumzia suala la ufisadi ambapo alidai jumla ya Shilingi Trilioni 2.5 Milioni zimepotea kutokana na ubadhirifu kwa mujibu wa Ripoti ya CAG 2023/2024, pamoja na kupotea kwa baadhi ya Watu.

Image with Link Description of Image

Akichangia, alikatishwa mara mbili kwa taarifa kutoka kwa Mbunge wa Kaliua Tama na Waziri wa Mambo Patrobas Katambi, Mwenyekiti wa Bunge, Cecilia Pareso alipomtaka Ado kukaa, alijaribu bila mafanikio kuomba muda wa ziada wa dakika moja kutokana kuingiliwa mara kwa mara kwa taarifa na kupotezewa muda wake.

Spika Zungu amemweleza Ado kuwa anasamehewa kwa sababu ni Mbunge mgeni lakini asipobadilika Spika atalazimika kuchukua hatua za kinidhamu za kikanuni dhidi yake.