Tangazo la kazi MDAs & LGAs 2024 – Nafasi 6,257
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma, kwa niaba ya Wizara, Idara zinazo jitegemea, Wakala za Serikali, Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa (MDAs & LGAs) anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi Elfu sita, mia mbili, hamsini na saba (6,257) kama ilivyoainishwa katika tangazo hili.